ads

Friday, March 30, 2018

Wasanii Roma Mkatoliki, Pretty Kind watolewa 'kifungoni'

WASANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ibrahim Musa, maarufu kama 'Roma Mkatoliki' na Suzan Michael 'Pretty Kind' wamesamehewa adhabu ya kutojihusisha na muziki kwa miezi sita waliyokuwa wanatumikia baada ya kukiri makosa na kuomba msamaha.
Wasanii hao walifugiwa kutojihusisha na masuala ya sanaa na Serikali baada ya kufanya kazi zilizo kinyume maadili ya taifa. Tofauti na msanii Pretty Kind ambaye ameruhusiwa kuendelea na kazi yake ya muziki baada ya kuwa amekamilisha taratibu zote ikiwamo kujisajili BASATA, Roma yeye ametakiwa kukamilisha kujisajili ili apate cheti cha utambulisho kama msanii.
Aidha, mwanamuziki huyo mahiri wa muziki wa kughani amevitaka vituo vya redio na luninga kutoendelea kuupiga wimbo wa Kibamia ambao ndiyo hasa ulimuingiza matatani kutokana na maudhui yake.

Katika kikao cha walichokaa wasanii hao, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri, Juliana Shonza, wajumbe wa bodi ya filamu na chama cha wanamuziki wa Bongofleva, Roma alitakiwa kuurudia wimbo huo na kuusahihisha ndipo uendelee kuchezwa kwenye vituo vya redio na luninga. Kwa upande wake Waziri Mwakyembe ameagiza wasanii kuzingatia maadili ya taifa Katika kazi zao. Pia amewakumbusha wasanii kujisajili BASATA ili watambulike

No comments:

Post a Comment