ads

Saturday, March 24, 2018

Ngoma, Tambwe wainogesha Yanga

imeandikwa na Tosko Salehe
KOCHA wa Yanga George Lwandamina amesema kurejea mazoezi kwa washambuliaji wake wawili Donald Ngoma na Amissi Tambwe kuna mpa matumaini ya kufanya vizuri kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Walayti Dicha ya Ethiopia.
Yanga imeangukia kwenye michuano ya Caf, baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na timu ya Township Rollers ya Botswana kwa jumla ya mabao 2-1.
Akizungumza na gazeti hili Lwandamina, alisema kurejea kwa wachezaji hao kumeongeza matumaini ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo ambao amepania kupata ushindi mnono katika mchezo wao wa kwana utakaopigwa hapa nyumbani Tanzania.
“Unajua katika mchezo huo tutawakosa wachezaji watatu muhimu, Papy Kabamba, Said Makapu na Obrey Chirwa ambao ni wachezaji muhimu lakini furaha pekee ni kurejea kwa wachezaji hao waliokuwa majeruhi kwa muda mrefu naamini watakuwa na mchango mkubwa kuelekea hatua ya makundi,” alisema Lwandamina.
Kocha huyo alisema baada ya kupona na kuanza mazoezi amepanga kutumia muda uliobaki kuwapa mazoezi ili kuimarisha viwango vyao na kuweza kuisaidia timu katika mchezo huo ambao ushindi kwao ni muhimu.

Kwa mujibu wa Caf, Yanga itaanzia nyumbani kati ya Aprili 6 au 7 na mchezo wa marudiano utapigwa Ethiopia baada ya siku 10, hivyo wawakilishi hao wa Tanzania wanakazi kubwa kuhakikisha wanaitumia vizuri nafasi ya kuanzia nyumbani.

No comments:

Post a Comment